Wednesday, 8 June 2016
ZITTO KABWE AITWA KITUO KIKUU CHA POLISI DAR.
KiKiongozi wa Chama cha ACT-wazalendo Zitto Kabwe ameitwa polisi. Kwa mujibu wa Taarifa alioituka kupitia ukurasa wake wa Facebook kuongozi huyo na mbunge wa kigoma mjini hajaeleza sababu za kuitwa huko. Aidha Msemaji wa Chama hichi Ado shaibu amethibitisha jutokea kwa tukio hilo na kwamba Zitto alipaswa kwenda jana ila mda ukawa umeisha na hivyo kutakiwa kufika leo na mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar. Zitto anaitwa polisi ikiwa ni siku moja baada ya kuhutubia mkutano wake wa Kampeni linda Demokrasia Huko Dar. Aidha Zitto Kabwe ni miongoni mwa wabunge waliotimuliwa bungeni kutohudhuria baadhi ya vikao kutokana na sababu mbalimbali za kimakosa, hata hivyo chama hicho kilikuwa na mkakati wa kufanya mikutano nchi nzima, zoezi ambalo limegonga mwamba baada ya hapo jana polisi kupiga marufuku mikutano yote ya hadhara nchini mpaka hapo itakapopewa kibali kutokana na sababu za kiusalama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment