Saturday, 9 July 2016

BAVICHA WAITANGULIA CCM DODOMA, WAISHIA RUMANDE

JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia viongozi watatu wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Taifa, kwa uchochezi na kuikashifu serikali. Pia viongozi hao wanadaiwa kuvaa fulana zenye maandishi demokrasia imenyongwa, huku nyingine zikiandikwa dikteta uchwara. Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha- Taifa, Patrobas Katambi, Katibu wa Bavicha-Taifa, Julius Mwita na Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Mbeya, George Tito. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema watuhumiwa hao watashikiliwa mpaka Jumatatu watakapofikishwa mahakamani. “Hawatadhaminiwa mpaka Jumatatu, watakapofikishwa mahakamani,” alisema. Kamanda Mambosasa alisema kitendo cha viongozi hao kuvaa fulana inayosema demokrasia imenyongwa, inamaanisha serikali inanyonga demokrasia, jambo ambalo ni la uchochezi.

No comments:

Post a Comment