Wednesday, 13 July 2016

HABARI TOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Bodi ya Mikopo imetoa orodha ya wanafunzi mbalimbali ambao hawakujitokeza ktk zoezi la uhakii la hivivi karibuni wanaofikia zaidi ya Elfu mbili, Kwa Taarifa hii bodi inawatalka wale wote ambao hawajajitokeza kuhakiki kufanya zoezi hilo ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 13 baada ya hapo atakayeshindwa atafutiwa mkopo wake rasmi na kutakiwa kurudisha aliokwishakopeshwa mara moja. Orodha ya wanafunzi ni 2,739 kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu ambao hawakuhakikiwa na ambao wanatakiwa kujitokeza ndani ya siku saba (07) kuanzia tarehe 13 Julai, 2016 ili kuhakikiwa katika sehemu watakazoelekezwa na vyuo husika. Ili kuona majina ingia http://olas.heslb.go.tz.

No comments:

Post a Comment