Wednesday, 8 June 2016
BAJETI KUU ZA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI HIZI HAPA
Nchi za Afrika ya Mashariki leo zimewasilisha bajeti zao za Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo kwa upande wa Tanzania waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango amewasilisha zaidi ya Shilingi Tilioni 29. Akiwasilisha bajeti hiyo waziri wa Fedha ameeleza kuwa matumizi yatkuwa zaidi ya Tilioni 16 na miradi ya maendeleo imetengewa shilingi tilioni 12. Katika bajeti hiyo pia baadhi ya bidhaa zimepanda ktk tozo la kodi ikiwemo bia na baadhi ya vinywaji. Aidha Uasajiki wa namva binafsi za Magari na pikipiki umepanda, lakini pia kushuka kwa kodi kutoka 11% kwebda 9%(PAYE). Nchini Kenya Waziri wa Fedha wa nchi hiyo amewasilisha bajeti ya nchi hiyo ambayo miundombinu imepewa nafasi kubwa.
Katika nchi ya Uganda waziri wa Fedha wa Nchi hiyo amewasilisha bajeti ya nchi hiyo inayofikia fedha za nchi hiyo shilingi tilioni 26, Huku ktk Nchi ya Rwabda Waziri wa Fedha wa Nchi hiyo akiwasilisha bajeti ya Serikali ya Raisi Kagame huku akisema bajeti hiyo umepunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa wahisani.
Nchini Tanzania bajeti kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ilikuwa tilioni 22 huku ile ya mwaka wa Fedha 2014/15 ikiwa ni shilingi tilioni 19 na zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment