Wednesday, 8 June 2016

ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI MKOANI ARUSHA AHUKUMIWA RASMI

Mahakama ya hakimu mkazi mkoani Arusha imemhukumu Isack Abakuki kifungo cha miaka 3 leo au faini ya Sh. 7 Milioni kwa kosa la kumtukana Raisi Magufuli kwa njia ya Mtandao wa Facebook. Kesi hiyo ilitolewa maamuzi leo baada ya mtuhumiwa huyo kukiri kosa mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama hiyo. Abakuki amekubali kulipa faini ya milioni 7 kwa awamu mbili yaani july 8 na August 8 mwaka huu ambapo atalipa shilingi milioni 3.5 kwa awamu hizo zote ili kuepuka kifungo hicho cha miaka mitatu jela.

No comments:

Post a Comment