Wednesday, 8 June 2016
ZITTO KABWE AHOJIWA NA POLISI
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe alihojiwa kwa saa 3 Mfululizo na Mkuu pamoja na Kaimu mkuu wa Upelelezi kanda maalum ya Dare-es-Salaam. Kiongozi huyo ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini alihojiwa kutokana na hotuba yake alioitoa katika viwanja vya Zakheim Mbagala Dare-es-Salaam, katika kile alichokiita ni Operation Linda Demokrasia. Juzi Jumapili Zitto alihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho huku akituhumu baadhi ya mambo ambayo kwa upande wake anaona hayaendi sawa Serikalini na pia Suala la Wabunge wa upinzani kusimamishwa baadhi ya Vikao bungeni akiwemo yeye mwenyewe.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuhojiwa Zitto amesema kuwa kuhojiwa kwake kuna lengo lakuunyamazisha upinzani na kwamba hajaona umuhimu wa suala hilo kwani muda polisi waliotumia kumhoji wangeweza kuutumiakupambana na ujambazi. Aidha ameeleza kuwa kuhusu suala la kuendelea na mikutano nchi nzima halipo tena baada ya katazo la polisi ila wanajaribu kuangalia utaratibu wa kisheria ili kuangalia tafsiri ya mahakama kuhusiana na suala hilo.
Wakati huo huo, Polisi mkoani Shinyanga jana iliusindikiza Msafala wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti Mh. Freeman Mbowe kupita moja kwa moja mkoani humo bilakuingia ofisi za Chadema, Polisi wameendelea kusimamia agizo la juu la Chombo hicho cha Ualama wa Raia kilichopiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa kote nchini mpaka hapo litakapotoa kibali tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment