Wednesday, 8 June 2016
WABUNGE WANAOSAIN POSHO NA KUONDOKA KUKIONA
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Akson ameagiza kutolipwa posho kwa wabunge wote watakaoingia bungeni na kusaini na kuondoka bila sababu maalum. Naibu spika alisoma muongozo huo kwa kurejra kanuni ya mwaka 2006 iliyokwisha toa maamuzi juu ya wabunge wa aina hiyo. Hayo ameyasema wakati wa kusoma miongozo mbalimbali iliyowasilishwa na wabunge juu ya suala hilo mara baada ya waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha hotuba yake hapo jana jioni. Wabunge wa upinzani wamekuwa wakisusia vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo huku wakiingia bungeni na kusaini posho na kuondoka kuanzia mwanzoni mwaa mwezi huu.
Katika hatua nyingine Naibu Spika ametolea ufafanuzi juu ya uvumi unaoenea kuwa Spika Job Ndugai anaumwa. Akitoa ufafanuzi Naibu Spika ameeleza kuwa Spika hali yake ni Nzuri na kwamba yuko nchini India kwa uchunguzi wa afya yake kwa mujibu wa Daktari wa kiongozi huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment