Friday, 10 June 2016

MBUNGE WA MBEYA MJINI MATATANI

Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Acksoni Mwansasu ameitaka kamati ya Bunge ya Haki na Maadili kumchunguza mara moja mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi-SUGU kwa tuhuma za kuwanyooshea kidole cha kati wabunge wa CCM June 6 Mwaka huu. Sugu anadaiwa kutenda kosa hilo nje ya Ukumbi wa bunge mjini Dodoma. Aidha Naibu Spika ameitaka kamati hiyo kumpa adhabu kali mbunge huyo iwapo atapatikana na hatia ya kutenda kosa hilo.

No comments:

Post a Comment