Friday, 10 June 2016

ZITO AWACHOKONOA WABUNGE WENZAKE

Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amependekeza kukatwa kodi kwa posho za wabunge zinazofikia sh. 220,000/- kwa siku sawa na milioni 200 kwa mwaka ili kupanua wigo wa Mapato ya Serikali. Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma mjini aliyasema hayo juzi katika mjadala wa kuchanganua bajeti ulioendeshwa na Taasisi moja Jijini Dar. Zitto ameeleza kuwa anaona ni wakati sahihi wa posho hizo kukatwa kwani kwa mda mrefu zimekuwa zinatolewa bure kitu ambacho si sahihi.Zitto ni mbunge pekee katika bunge la 10 aliyekataa kupokea posho hiyo ya vikao na kupendekeza iondolewe kabisa zoezi ambalo hata hivyo liligonga mwamba Katika bajeti iliyosomwa juzi tar 08/06/2016 Serikali ilieleza kuwa kutakuwa na makato ya kodi katika kiinua mgongo cha wabunge kinachotolewa kila baada ya miaka 5 ambacho kwa mwaka 2015 kilifikia sh. 172 milioni bila kukatwa kodi. Zito alilaumu suala hilo kuwa limechelewa kwani kiinua mgongo hicho kitatolewa 2020. Wakati Zitto akiyasema hayo baadhi ya wabunge wamelalamikia kitendo cha serikali kukata kodi katika fedha hizo wakidai itawageuza kuwa ombaomba, na baadae kupendekeza kuwa iwapo serikali itakomaa na msimamo wakeni vyema kodi hiyo ikatwa kwa viongozi wote wa kisiasa. Wa kati huo huo baadhi ya viongozi wa chadema na ukawa wamesema kuwa suala lakusitishiwa posho za vikao vya bunge haiwatishi kwa kuwa wanahoja yamsingi. Naibu spika alitoa uwamuzi wa wabunge wote wa upinzani kutolipwa posho kwa kususia vikao, ambapo hata hivyo jana baadhi yao walisalimu amri na kuingia kusoma hotuba yao ya wizara ya fedha kupitia kwa naibu waziri kivuli wa wizara hiyo Davidi Silinde.

No comments:

Post a Comment