Saturday, 11 June 2016

UFAFANUZI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU

Ofisi ya Raisi-TAMISEMI imekanusha taarifa potofu zilizoenea katika baadhi ya vyombo vya habarikuhusu kutoajiriwa kwa walinu wa biashara na sanaa kwa mwaka 2015/2016. Taarifa zirifa zilizosamvaa katika vyombo mbali mbali vya habari na na umma zinaeleza juwa serikali imesitisha ajira kwa walimu hao baada ya kuwa na ziada ya walimu wa sanaa na biashara zaidi ya elfu 78 katika shule za sekondari nchini, na baadala yake serikali itaajiri tu walimu wa sayansi na hisabati. Taarifa ilitolewa na TAMISEMI kupitia kitebgo chake cha mawasiliano serkalini jana imewataka watanzania kupuuza taarifa hizo na kwamba mchakato wa kuajiri upo palepale na utakapokuwa tayari utatangazwa kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI. Aidha TAMISEMI imewataka wote wanaohusika na kuandaa taarifa hizo potofu kuacha mara moja vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na Sheria.

No comments:

Post a Comment