Friday, 10 June 2016
CHADEMA YAJIFUNGIA NDANI KUJADILI ZUIO LA POLISI
Chama cha CHADEMA kimejifungia ndani kwa siku 2 kikijadili hatua ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya kisiasa nchini kwa sababu za kiusalama hadi hapo kibali kitakapotolewa tena mkutano huo wa ndani uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh. Freemani mbowe ulikaliwa jana katika ukumbi wa Mandela katika Hotel ya Gold Crest jijini mwanza, ambapo Mbowe alipoulizwa na waandishi wa habari alisema watatoa tamko leo baada ya mkutano wao wa Usiku katika hotel hiyo. June 7. Jeshi la polisi lilipiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa baada ya vyanzo vyake vya kiinteligensia kugundua kuwa mikutano hiyo inaweza kutumika kuwahamasisha wananchi kuvunja sheria za nchi na hivyo kupelekea vurugu. Aidha jeshi hilo lilisema kuwa kuna uwezekano wa vyama kufanya majibizano katika muendelezo wa mikutano hiyo kitu kinachweza kuibua vurugu pia.
Wakati jeshi hilo likipiga marufuku mikutano hiyo tayari chama cha ACT wazalendo kilikuwa kimeanza mkutano wake wa kwanza Jumapili jijini DareesSalaam ktk viwanja vya Zakheim Mbagala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment