Sunday, 5 June 2016

WANAFUNZI 130 CHUO KIKUU TUMAINI MBEYA KTK HATIHATI YA KUTOFANYA MITIHANI YA MWISHO

Wanafunzi 130 ktk Chuo kikuu cha Tumaini Mkumira Tawi la Mbeya ktk course ya Afya ya jamii wako ktk hathati ya kutofanya mitihani yao ya mwisho baada ya kukosa Usajiki kutoka NACTE. Eanafunzi hao walishuhudiwa jana na Mwandishi wa ITV wakiwa nje ya majengo ya utawala wa chuo hicho wakitaka kujua hatima yao. Wanafunzi hao waliobakiza Mwezi kumaliza chuo, wamekilaani chuo hicho kwa vitendo kinavyowafanyia na kuitaka Serikali kuingilia kati suala hilo. Hata hivyo mwandishi wa Itv aliingia ndani kupata maelezo ya utawala wa chuo hicho ambapo alimkuta mkuu wa Chuo hicho ambaye hata hivyo hakuwa tayari kuzungumza chochote.

No comments:

Post a Comment