Sunday, 5 June 2016
RIPOTI YA BANK KUU YATUA KWA RAIS MAGUFULI
Bank kuu ya Tabzania(BoT), imemaliza kuandaa ripoti ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli wakati akifanya ziara ktk benki hiyo mwezi March Mwaka huu. Wakati akifanya ziara hiyo rais Magufuli aliagiza kupitiwa upya kwa wafanyakazi wa bank hiyo wapatao 1391 akidai kuwa ni wengi saba hivyo taasisi hiyo ya umma ipitie upya na kuona uwezekano wa kupunguza wale wasiokuwa na kazi za muhim ambazo zinaweza kufanywa na watu wachache. Jana gavana wa Bank hiyo Prof. Ndulu aliiambia nipashe kuwa ripoti hiyo iko tayari na isshaapelekwa ktkmamlaka husika na kwamba wao ndio jukumu lao na sio kuchapisha kwenye magazeti. Taasisi hiyo inatuhumiwa kuwa na majina ya watoto wengi wa vigogo waliopo seerikalini ama waliokwisha fanya kazi serikalini ktk awamu mbalimvali hivyo huenda nafasi hizo walizipata kwasababu ya ndgu zao. Alipoulizwa kuhusu majina hayo prof. Ndulu alisema hayo majina yapo na si ajabu. Kamamtu anasifa za kuajiriwa si makosa na wala kutokea ktk jina kubwa haiwez kuwa sababu ya kutoajiriwa. Baadhi ya watumishi wa Taasisi hiyo wamekuwa na wasiwasi wa kutumbuliwa endapo itabainika kuwa kazi zao zinaweza kufanywa na watu wachache kama alivyopendekeza raisi ktk ziara yake hapo mwezi March 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment