Wednesday, 1 June 2016
WALIOANZISHA MGOMO UDSM KUADHIBIWA
Rais Wa Tanzania anatarajiwa kutembelea Chuo kikuu cha DaresSalaam leo. Ktk Ziara hiyo Rais anatarajiwa kuzindua ujenzi wa Maktaba Mpya Chuoni hapo. Chuo kikuu Cha Dsm ndio chuo kikuu ambacho mh. Rais amepata elimu yake pale kuanzia ngazi ya Shahada hadi Shahada yaUzamivu(PhD), miezi michache iliyopita rais alimchagua rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Kikwete kuwa mkuu Mpya wa Chuo hicho.
Rais Magufuli anatembelea chuo hicho ikiwa ni siku mbili tu tangu wanafunzi wa Chuo hicho wagoke wakidai fedha zao za kujikim, wanafunzi hao juzi walionekana wakitembea chuoni hapo huku wakiwa wanaimba kauli mojawapo ya Mh. Rais wakati akitafuta ridhaa mwaka 2015 wakisema" Katika serikali yangu mimi wanafunzi wakigoma atakayewajibika ni bodi ya Mikopoo na sio wanafunzi". Hata hivyo mamlaka chuoni hapo zimesema zinaendelea kufatilia suala hilo kujua waazilishi wa mgomo huo, kwani kwa Mujibu wa sheria ndogo za chuo ni marufuku kwa mwanafunzi kuanzisha mkusanyiko usio halali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment