Thursday, 2 June 2016
WABUNGE WALIOSIMAMISHWA VIKAO BUNGENI KUONGEZEWA ADHABU
Wabunge wa upinzani waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge huenda wakakutana na adhabu nyingine ya kukatwa mshahara na posho. Kamati ya bunge ya haki na maadili ambayo ndio inayosimamia nidhamu bungeni imetoa adhimio hilo kama nyongeza ya adhabu kwa wabunge hao ambao waliomba mwongozo wa kiti kwa jambo lilokwisha tolewa maamuzi. Juzi bunge liliwasimamisha kuhudhuria vikao mbalimbali wabunge wa upinzani akiwemo Tundu Lisu, Halima Mdee na Zitto Kabwe. Walipoulizwa baadhi yao walidai kuwa hawatambui suala hilo na wala hawakuliskia kwani hawajapata hata barua ya kusimamishwa bunge. Naye mbunge Heche amesema kuwa haoni shida kukatwa mshahara na posho ktk suala hilo kwani haki inaminya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment