Monday, 6 June 2016
WALIMU WASTAAFU WA SAYANSI KUAJILIWA KWA MKATABA MAALUM.
Serikali imesema kuwa itafanya mpango maalum wa kuajili walimu wa Sayansi hata waliostaafu iki kutatua tatizo la Walimu wa Sayansi nchini. Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. Suoeimani Jaffo amesema leo bungeni Dodoma kuwa wataangalia utaratibu huo ili kutatua tatizo hilo lililokubwa nchini. Aidha Mh. Jafo ameongeza kuwa wataangalia pia vijana waliosomea masomo menginine ya Sayansi na kuona kama wanawezakuwapa mafunzo ya Muda ya ualimu pia waweze kusaidia suala hilo. Amewataja watakaofikiriwa kuwa ni wale waliosomea Shahada za Kemia, Fizikia,na Hesabu ila sio walimu yaani Shahada ya Kemia. Akiongezeamajibu Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amesema kuwa kuna upungufu wa walimu wa kada hiyo zaidi ya elfu 22, na kwamba waliopo kwa sasa ni zaid ya elfu12 ktk shule za Sekondari nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment