Monday, 6 June 2016
MSANII DIAMOND AGUSWA NA SUALA LA WATOTO WA SHULE KUKAA CHINI, AAMUA HIVI.
Msani maarufu wa Bongo Flevor Nasibu Abdul-Diamond ametoa Madawati 600 ya shule za msingi ikiwa ni juhudi za kumuunga mkono mkuu wa Mkoa wa Dare-es-Salaam Paul Makonda. Diamond alikabidhi madawati hayo leo kwa Mkuu huyo wa mkoa. Akizungumzaa baada ya kupokea mchango huo kutokakwa mkurugenzi huyo wa WCB, Makonda alifurahishwa na kitendo cha msanii huyo kwa kuichangia Elimu. Toka kuanzishwa kwa mpango wa elimu bure kumekuwa na changamoto ya madawati hususani ktk shule za msingi, tatizo ambalo kwa sasa linashughulikiwa kwa kasi kubwa na viongozi mbalimbali ktk ngazi mbalimbali za Serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment