Thursday, 2 June 2016

RAMADHAN KAREEM

Tar,07/06/2016, Waisilam Wa Tz na Maeneo Mengine wanatarajiwa kuanza Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani au Mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ktk Mwezi huu waisilamu au waumini wa Dini ya Kiisilamu hutakiwa kufunga kati ya siju29 hadi 30, kwa mantiki hii kwa kuwa kwa Mujibu wa Kanuni za Dini ya kiisilam, waumini hufunga kwa kuuona na kufungua kwa kuuona mwezi baasi Sikukuu ya Eid-Elfitry inatazamiwa kuwa kati ya Tar 06/07 au tar 07/07/2016. Funga ktk Dini ya Kiisilam ni kitu kilichosisitiziwa sana, kwani ni Miongoni mwa Nguzotano kuu za Dini ya Kisilamu, hivyo kutofungaMwezi wa Ramadhani inamaanisha umevunja nguzo moja ktk Dini hii.Katika kipindi hiki waumini Wa Dini ya kiisilamu hutubu madhambi yao, na kumuomba Muumba awaondolee mitihani mbali mbali ktk Maisha. Muumini wa,Dini ya Kiisilamu napofunga Mwezi huu, huzuiwa kufanya Mambo mbali mbali yakiwemo kunywa,kula,kutoa Lugha ya dhihaka na yenye kuudhi,kusengenya,jutamani na kujihusisha na Masuala ya Mapebzi, Funga pia inahusisha ufungaji wa kila kiungo mwilini ikiwa ni pamoja na kuyazuia macho kuangalia vitu visivyofaa kama vila pichazisizofaa,mavazi ya uchi, pia kuyazuia maskio kusikiliza vitu visivyofaa kama muziki,stori za kusengenya,fujo, na kadhalika. Ktk Dini hii ya Kiisilamu yote yaliyotajwa kwa ujumla yamekatazwa ktk vipindi vyote ila hapa ukiwa umefunga ni baadhi ya mambo ambayo yatatengua Swaumu yako. Pia waisilamu wameaswa kuhakikisha wanatimiza Swala zote ktk Mwezi huu na ktk Maisha yao yote hapa Duniani. Mwezimungu Mtukufu Aijaalie Swaumu ya Mwaka huu iwe ni Yenye kuwa na Daraja kubwa kwa Waumini wa Dini ya Kiisilamu Tz na Dunia kwa Ujumla..INSHAALLAH,RAMADHAN KAREEM.

No comments:

Post a Comment