Friday, 17 June 2016

WABUNGE 2 WA CHADEMA WASIMAMISHWA TENA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

Idadi ya wabunge waliosimamishwa vikao vya bunge imeongezeka baada ya leo Naibu spika Dk. Tulia Aksoni kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili wa viti maalum wachadema. Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao ni Suzani Lymo vikao 5 na Anatropia Theonest vikao vitatu. Suzani Lymo amesimamishwa vikao hivyo kwa kuongea uongo bungeni kuwa serikali imeagiza magari 777 ya washawasha wakati magari hayo ni jumla ya magari ya shughuli mbalimbali za jeshi hilo na sio washawasha tu. Anatropia amesimamishwa vikao 3 baada ya kuongea uongo kuwa Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya makaazi Wiliamu Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi wa Dar wakati akiwa mkuu wa mkoa huo. Mwishoni mwa may, wabunge 7 walisimamishwa vikao mbalimbali kwa kugundulika kuleta vurugu bungeni January mwaka huu wakati wa mjadala wa kutaka bunge lirushwe moja kwa moja na Tv ya Taifa wakati Serikali ikitoa hoja ya kurusha bunge hilo kwa kipindi maalumu cha saa 4 usiku.

No comments:

Post a Comment