Friday, 17 June 2016
Prof. Lipumba agonga mwamba katika juhudi za kuutaka uwenyekiti CUF
Chama cha CUF kimesema kuwa mkutano mkuu wa chama hicho kupata viongozi wapya uko palepale na kwamba Lipumba kama anataka uwenyekiti achukue upya fomu ya kugombea. Mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama hicho Shaweji Mketo amesema kuwa Fomu za kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo uwenyekiti zishaapelekwa wilayani na kwamba kwa ngazi ya makamu mwenyekiti.na Mwenyekiti itakuwa July 1, hadi 20.
Juzi Lipumba alisema amemuandikia katibu mkuu wa chama hicho barua ya kutengua kujiuzulu kwake ili arejee kwenye nafasi ya uwenyekiti.
Kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusu kuomba kurejea huko ambapo baadhi ya wanachama wametafsiri hatua hiyo ya Prof. Lipumba kama njama ya kutaka kukimaliza chama hicho, kwani sababu zilizomfanya ajiuzulu ziko palepale ikiwemo Lowasa kuwa UKAWA kwa hiyo mrejeo wake huo kutiliwa mashaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment