Tuesday, 7 June 2016

TAARIFA KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu imekanusha vikali taarifa zauongo zilizoenea ktk mitandao mbalimbali ya kijamii zikielezea kuusu vigezo vya kupata mkopo mwaka huu wa 2016/2017. Pamoja na maelezo mengine taarifa hiyo inaeleza kuwa watakaopata mkopo ni watahiniwa watakaopata daraja la kwanza na la pili kwa Kidato cha sita. Aidha taarifa hiyo ya uongo imeongeza kuwa watu wa diploma hawatapata mkopo. Hivyo bodi inapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na kwamba mchakato wa kutoa mikopo haujatangazwa bado na ukiwa tayari wadau wote watajulishwa.

No comments:

Post a Comment