Monday, 6 June 2016
BAADHI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU ST. JOSEPH WASITISHIWA MIKOPO
Serikali imewafutia mikopo wanafunzi wote wa mafunzo ya ualimu wa programu maalumu ya miaka 5 wa chuo kikuu Cha Mt. Joseph Tawi la Arusha kilichofutiwa usajili Mapema mwezi Febr Mwaka huu. Taarifa iliotolewa kwa waandishi wa habari na Kaimu Katibu mkuu Wizara ya elimu hapo jana imeeleza kuwa wanafunzi hao wamefutiwa mikopo hiyo baada ya kubainika kuwa hawana sifa ya kupokea mikopo hiyo. Aidha Prof. Simon Msanjila ameongeza kuwa wanafunzi hao hawataruhusiwa kusoma shahada, na baadala yake wasome Cheti na Diploma na wakushaamaliza wanaweza omba upya shahada. MweziFebuary mwaka huu Serikali ilikifutia chuo hicho usajili baada ya kubainika kutokuwa na sifa ya kufundisha shahada ya ualimu na piakuchukua wanafunzi wasio na sifa. Aidha kutokana na uchambuzi huo imepelekea hata baadhi ya wanafunzi waliohamishiwa vyuo vingine kutopata mikopo yao kwa wakati ili bodi ichambue wenye sifa za kupokeamkopo, ambapo mwezi May 31, bodi hiyo iliweka tangazo linaloonesha kuwa mchakato wa kuwapa wanafunzi wenye sifa umekamilika na kuwataka kuwa wavumilivu kwa muda wakati bodi ikiziproses fedha zao kwendaktk vyuo walikohamishiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment