Wednesday, 15 June 2016
SIMU FEKI KUZIMWA RASMI KESHO
Serikali imesema kuwa zoezi la kuzima simu feki litakuwa palepale hapo kesho. Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tz-TCRA wakati akizungumza na waandishi wa habari mapemaleo Jijini Dar. Kwa Mujibu wa kaimu mkurugenzi huuo bwana James Kilaba amesema kuwa wameshaatoa mda mwingi na elimu juu ya simu hizo hivyo hakuta kuwa na nyongeza ya muda. Serikali ilitoa muda wa miezi sita kuhakikisha wananchi hawamiliki simu feki ili kupunguza madhara yatokanayo na simu hizo. Mhandisi Kilaba ameeleza kuwa simu zitakazozimwa zihifadhiwe mazingira salama. Pia amesema kuwa hata zile zilizobadilishwa flashi zitazimwa tu, na kwamba kubadili flashi ni kosa la jinai na mtu akigundulika huweza kupata adhabu hadi ya kifungo cha miaka kumi.
Serikali inatarajia kuzima simu hizo kesho tar 16 majira ya saa 6 usiku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment