Wednesday, 15 June 2016

LUSINDE: WABUNGE WA CHADEMA WAMENITUMA NIMWAMBIE MBOWE AWARUDISHE BUNGENI.

Mbunge wa mtera Livingstone Lusinde amesema kwamba wabunge wa upinzani hususani chadema wamemtuma amwambie mwenyekiti wao Freeman Mbowe awarudishe bungeni kwani yeye ndio anawafanya watoke bungeni. Lusinde amemweleza naibu Spika wa bunge kuwa hakuna mtu dikteta katika nchi hii zaidi ya mbowe kwani wabunge wa chadema wamesema anawaburuuza kutoka bungeni ila wao hawataki kususia vikao. Lusinde ameeleza kuwa wabunge wa chadema wako kwenye chai wameniomba kuwa wao hawawez kumuambia mbowe, hivyo awasemee. Akijibu hoja hiyo, Naibu spika ameeleza kuwa wabunge wote wanaosusia vikao wanasusia kwa utashi wao na wala sio msukumo wa mtu yeyote.

No comments:

Post a Comment