Wednesday, 15 June 2016

BASI LA TAHMEED, TANGA-DAR LAUNGUA KWA MOTO

Basi la Kampuni ya TAHMEED linalofanya safari zake kati ya Tanga na Dar limeteketea kwa moto. Basi hilo liliteketea likiwa katika barabara ya Chalinze Segerea likiwa limesimama, taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kwamba, basi hilo liliungua wakati limesimama baada ya abiria mmoja kuomba kuchimba dawa, ndipo abiria wengine waliposikia harufu ya tairi likiungua ndipo wakashuka. Taarifa zinaeleza kuwa, katika ajali hiyo, hakuna abiria aliyefariki wala kujeruhiwa, bali mizigo ya abiria iliokuwa ndani ya gari hilo imeteketea kwa moto yote.

No comments:

Post a Comment