Sunday, 12 June 2016

SERIKALI YAKIFUNGA CHUO CHA KILIMO NA MIFUGO MBEYA POLYTECHNIC

Serikali kupitia NACTE imekifunga Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Mbeya Polytechnic kilichopo jijini mbeya. Taarifa zilizopatikana chuoni hapo zinaarifu kwamba vilio vilitawala chuoni hspo baada ya tamko la kukifunga chuo hicho kilichokuwa kikitoa mafunzo ya Mifugo na kilimo. Tangazo la kukifunga chuo hicho lilisomwa jana na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala kwa niaba ya NACTE akieleza kuwa sababu za kufungwa kwa chuo hicho ni kuwa na mapungufu mengi na pia kudahili wanafunzi waio na sifa. Mkuui huyo wa mkoa ametolea mfano kuwa wanafunzi waliokuwa chuoni hapo zaidi ya 300 wenye sifa ni 89 tu. Baadhi ya wanafunzi wameitaka serikali kuingila kati suala hilo ili walipwe fidia, kwani baadhi yao wanamiezi miwili wamefuatilia vyeti huku wakizungiushwa tu kumbe vyeti havipo. Mkurugenzi wa Chuo hicho ameomba radhi na kusema kuwa wanafunzi wawasamehe tu kwani kazi ya kuendesha chuo ni ngumu. Serikali imeahidi kuwahamisha baadhi ya wanafunzi wenye sifa kwenda vyuo vingine ili kuendelea na masomo yao.

No comments:

Post a Comment