Sunday, 12 June 2016
KONGAMANO LA KUJADILI BAJETI LA ZITOKABWE LAGONGA MWAMBA
Polisi mkoa wa Dar, wamezuia kongamano la kujadili bajeti lililokuwa liendeshshwe na Chama Cha ACT Wazalendo ikiwa Zitto Kabwe alitarajiwa kuwa msemaji mkuu wa kongamano hilo leo saa7 mchana katika Ukumbi wa LAPF millenium Tower Kijitonyama Dar. Taarifa kutoka ndani ya ACT zinaeleza kuwa polisi walianza kuzingira eneo hilo kuanzia saa6 mchana ambapo shughuli ilitakiwa kuanza saa7 mchana. Wasemaji wengine katika kongamano hilo walitarajiwa kuwa Mwenyekiti wa ACT wazalendo Mama Anna Mghwira Na Prof. Kitila Mkumbo, Mhadhiri UDSM na mwanachama wa Chama hicho. Taarifa iliandikwa katika ukurasa wa Facebook wa Mama Mghwira imeeleza kuwa Chama kitakutana leo jioni makao makuu ya Chama Kijitonyamakwa Taarifa zaidi. Hakuna taarifa zozote za zuio hilo kutoka uongozi wa polisi.
Hivi karibuni Polisi nchini ilipiga marufuou mikutano yeyote ya kisiasa nchini kwa sababu za kiusalama mpaka hapo taarifa itakapotolewa tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment