Saturday, 11 June 2016
CHADEMA YATINGA MAHAKAMA KUU KUPINGA AMRI YA POLISI KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA KWASABABU ZA KIUSALAMA
Chama cha CHADEMA kimefungua kesi katika mahakama kuu kanda ya mwanza kupinga amri ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya kisiasa nchini kwa sababu za kiusalama mpaka hapo litakapojiridhisha na hali ya usalama na kutoa kibali tena. Kesi hiyo ilifunguliwajana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe akiwa na viongozi wengine wa chama hicho. Baada ya kufungua kesi hiyo, Mbowe alisema wamefungua kesi hiyo baada ya kuona uhuru wa vyama vingi unaminywa. Kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016 ilifunguliwa dhidi ya kamanda wa polisi Kahama, Geita, Mwanasheria mkuu wa Serikali na Kamishina wa Mafunzo na Operasheni polisi Makao makuu. Mbowe ameeleza kuwa hawwezi angalia demokrasia ikinyang'anywa hivyo wameenda mahakamani kutafuta haki yao. Hivi karibuni jeshi la polisi lilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kwa sababu za kiusalama. Kesi hiyo inatarajiwa kupangiwa Jaji Siku ya Jumatatu tar13/06/2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment