Wednesday, 29 June 2016

SABABU ZA KUTUMBULIWA NDANI YA SAA 24 KWA MKUU WA WILAYA MTEULE-IKUNGI SINGIDA HIZI HAPA

Rais Magufuli amesema kuwa jina la bw, Fikiri said lilikosewa kutajwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Ikungi-Singida na kwamba mkuu halali wa wilaya hiyo ni Bw. Miraji Mtaturu katibu wa ccm Mkoa wa Mwanza. Jina la bwana saidi lilitajwa katika orodha ya wakuu waoya wa wilaya Juzi kabla ya kutenguliwa ndani ya saa 24 na Rais. Wakuu wote wa wilaya walioteuliwa wameapishwa leo Ikulu Dar. Hata hivyo kulikuwa na fununu kwamba Bw, Said baada ya kupata uteuzi huo aliwasiliana na viongozi wa ikulu kuomba aondolewe kitu ambacho raisi amesema sio kweli. Wakati huo huo, Taarifa kutoka mahakama kuu kanda ya Arusha zinaarifu kuwa Mahakama hiyo imetengua ubunge wa Mbunge wa Chadema Onesmo Ole Nangole wa Longido baada ya kuthibitisha kuwa ubunge huo ulipatikana kimakosa. Nangole analiwakikisha jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA, hivyo mahakama imeagiza kurudiwa upya kwa uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment