Wednesday, 29 June 2016

CHADEMA YAPATA PIGO ARUSHA

Chama cha CHADEMA, kimepata pigo baada ya mahakama kuu kanda ya Arusha kutengua ubunge wa Mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole hapo jana. Kwa mujibu wa hukumu iliotolewa na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Bukoba, jaji huyo ameeleza kuwa baada ya kuoitia ushahidi wa pande zote mbili jopo la Majaji limegundua kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki. Mgombea wa CCM Dk. Kiruswa anayefanya kazi nchini Marekani aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Maarufu Lamwai, alilalamikia rafu katika uchaguzi huo ikiwemo maboksi ya kura kubebwa kwa kutumia magari ya Chadema, kutangazwa kwa matokeo baada ya yekutolewa nje ya chumba cha kuhesabia kura na kutumika kwa lugha ya matusi katika kipindi cha kampeni ikiwemo kuambiwa yeye si Mmasai bali ni Raia wa Marekani kutokana na kufanya kazi nchini humo. Onesmo Ole Nangole alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha kabla ya kuhamia CHADEMA akimfuata Lowasa Mwezi wa 9 mwaka jana na kugombea katika jimbo hilo na kupata ubunge huo kinyume na taratibu. Kesi hiyo ilianza kunguruma mwezi wa pili tar 29 mwaka huu ambapo imesikilizwa kwa miezi 4 hadi hukumu yake hapo jana. Huyu ni mbunge wa kwanza kupoteza ubunge wake katika kesi zote za Uchaguzi wa Ubunge mwaka huu ambapo karibia wote waliopeleka kesi za kupinga matokeo ya ubunge walipigwa chini akiwemo Kafulila,Wenje, Haines Kiwia, Lembeli na Steven Wasira na wengineo. Kwa Mujibu wa hukumu hiyo, sasa jimbo hilo liko wazi na uchaguzi utarudiwa tena. Akizungumza na waandishi wa habari, Onesmo Ole Nangole alisema kuwa hajaridhika na hukumu hiyo. Hata hivyo hakuonesha nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa chombo hicho kikuu cha kusimamia sheria na kutoa haki nchini.

No comments:

Post a Comment