Sunday, 5 June 2016

POLISI MWANZA YAUA MAJAMBAZI WATATU.

Polis jijini mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi wameua majambazi 3 leo ktk majibizabo ya Silaha ktk mapango ya milima ya Utemini Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza. Taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari umeeleza kuwa majambazi hao wamejuwa wakihusika ktk matukio mbalimbali ikiwemo kupora maduka ya Mpesa. Taarifa hiyo imeongeza kuwa mapambano hayo yalidumu kwa masaa15 kuanzia alfajiri ya leo na kwamba wamekamata bunduki moja aina ya SMG, na vitu mbalimbali ktk maficho hayo ikiwemo kofia, vyakula vilivyokuwa vikipikwa na majambazi hao pamoja na Kisu. Eneo hilo liko jirani kabisa na eneo ambalo mauaji ya watu kadhaa yametokeaktk msikiti mmoja Jijini humo.

No comments:

Post a Comment