Saturday, 4 June 2016

RAIS WA Z'BAR AITAHADHALISHA CUF.

Rais wa Zanzibar amesema kuwa hamuogopi mtu yeyote akiwemo Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Hamadi. Rais Shein amesema kuwa hamuogopi kiongozi huyo kwani hana Roketi wala vifaru vya kivita vya kufanya aogopwe na watu wengine. Dk Shein ameyasema hayo ktk Ziara yake inayoendelea visiwani humo akisema kuwa Maalimu seif ni Mwanasiasa kama yeye, tofauti ni kwamba Yeye ni Rais na Maalim ni Kiongozi wa Chama. Rais Shein ameongeza kuwa Maalimu amekuwa akizungumza maneno ya uchochezi lakini vyombo vya Dopa vinashighulikia suala hilo na akipatikana na hatia atahukumiwa kama watu wengine, "Urais kama kuna mtu anautaka, hana budi kuchaguliwa, ila kwa sasa Rais ni mimi, hivyo simuogopi mtu yeyote na kwamba atakayekiuka sheria za nchi ataadhibiwa kama Raia wengine" Dk Shein aliongeza. Jeshi la polisi Visiwani humo linamhoji kiongozi huyo wa CUF kwa tuhuma za kutoa kauli mbalimbali zinazoashiria vutugu ktk mikutano yake ya hadhara anayofanya kuimarisha chama chake Visiwani humo.

No comments:

Post a Comment