Saturday, 18 June 2016

POLISI DODOMA YASAMBARATISHA MAHAFALI YA CHASO-UDOM

Polis mkoani Dodoma leo imeyasambaratisha mahafali ya CHASO (CHADEMA STUDENTS ORGSNIZATION)chuo kikuu cha Dodoma kwa kukosa kibali. Mahafali hayo yalikuwa yanafanyika katika ukumbi wa Afrikan Dreams ulioko Area D Mjini Dodoma Ambapo Mh. Sumaye alitarajiwa kuea mgeni Rasmi. Polisi kupitia Inteligensia yake walipata taarifa za mahafali hayo na kugundua kuwa hayakuwa na kibali na kuyasambaratidsha mara moja wakieleza kuwa mahafali pia ni miongoni mwa mikutano ya kisiasa iliopigwa marufuku. Polisi walipiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa nchini huku Chadema ikiwa imefungua kesi mahakama kuu kanda ya mwanza ambapo juzi Serikali kupitia mawakili wake waliiomba mahakamakufutilia mbali kesi hiyo kutokana na mapungufu ya kisheria yaliokuewa katika kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment