Monday, 20 June 2016
BAJETI KUU YA SERIKALI YAPITA KWA ASILIMIA MIA MOJA.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz, leo limepitisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/2017 kwa asilimia mia moja. Leo ndio siku ambayo bajeti hiyo ya shilingi Tz Tirion 29.5 imepitishwa rasmi kwa asilimia zote. Waziri wa Fedha na mipango alianza kwa kujibu hoja mmbalimbali za waheshimiwa wabunge ndipo baadae bajeti hiyo ilipopigiwa kura. Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango baada ya kupita kwa bajeti hiyo amewahakikishia watanzania kuwa inaenda kujibu kero zao mbalimbali ikiwemo Tz ya viwanda. Waziri mpango ameeleza kuwa, serikali itahakikisha makusanyo ya kodi ili kufikia malengo yake hayo.
Wakiongea na waandishi wa habari, wabunge mbalimbali wamesema bajeti hiyo inaenda kuibua na kujibu matatizo yote yalioainishwa katika Ilani ya CCM 2015/2020.
Akiongea na Mwananchi Digita Mbunge wa Mlalo Mkoani Tanga Mh. Abdallah Shangazi ameeleza kuwaqa, bajeti hiyo inaenda kutatua kero mbalimbali zilizoibuliwa ndni ya ilani ya ccm yamwaka 2015/2020 . Mheshimiwa Shangazi ameeleza kuwa anaona kuwa kero hizo zitaisha kutokana na msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya CCM ya kubana matumizi na kuhimiza ukusanyaji wa kodi. Mbunge huyo ametolea mfano kuwa toka kuingia madarani kwa serikali hii imekuwa ikikusanya si chini ya mapato ya Tirioni moja kwa mwez toka mwezi Novemba hadi sasa kiashirio kinachoonesha utekelezaji wa bajeti iliopita leo kwa kiasi kikubwa sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment