Sunday, 12 June 2016
OLE MEDEYE WA CHADEMA ATIMKIA UDP, ACHOSHWA NA TABIA ZA WABUNGE WA UKAWA.
Aliyekuwa kada wa CHADEMA na mbunge wa Arumeru.Magharibi Goodluck Ole Medeye ametimkia UDP leo mbele za mwenyekiti wa Chama hicho Mh. John Cheyo. Ole Medeye alikuwa mbunge wa Arumeru Magharibi kabla ya kutimkia Chadema mwaka 2015 mwishoni ambapo alipewa nafasi ya kugombea Uspika wa Bunge la Muungano na kushindwa vibaya na Mh. Job Yustino Ndugai alichaguliwa kwa kura nyingi kuongoza Bunge hilo.
Akitangaza uamuzi huo leo mbele ya Waandishi wa habari DareesSalaam Medeye ameeleza kuwa amechoshwa na Tabia za wabunge wa Upinzani kutomtii naibu spika wa bunge Mh. Dk. Tulia Aksoni. Medeye ameongeza kuwa yeye ni mtu anaependa kufuata kanuni hivyo hawezi vumilia tabia ya wabunge hao ya kususia vikao vya bunge.
Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vinavyoongozwa na Naibu spika lakini juzi waliweza kuwasilisha hotuba yao ya maoni na mapendekezo kuhusu bajeti ya serkali iliosomwa bungeni juzi tar8/06/2016 na waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Dk. Philip Mpango.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment