Sunday, 12 June 2016

ACT WATOA TAARIFA YA KUPOTEA KWA ZITTO KABWE

Kaimu katibu mkuu wa Chama cha ACT-wazalendo amesema kiongozi wao Zitto Kabwe hajulikani alipo. Kaimu katibu mkuu huyo amesema kuwa Zitto amekuwa akitafutwa na polisi toka jana usiku. Aidha kiongozi huyo ameongeza kuwa askari kanzu wanalibda nyumbani kwa kiongozi huyo na watu wake wa Karibu. Zitto alitarajiwa kuwa msemaji mkuu katika kongamano lililoandaliwa na Chama chake la kujadili bajeti ya serikali ya mwaka 2016/17 katika sura ya kizalendo lililokuwa lifanyike leo katika ukumbi wa millenium tower Kijitonyama Dar, leo kabla ya kongamano hilo kupigwa marufuku na polisi kanda maalum ya DAR, kwa kukosa kibali. Wasemaji wakuu webgine walikuwa ni Prof. Kitila Mkumbo, na Mwenyekiti wa Chama hicho Mama Anna Mghwira.

No comments:

Post a Comment