Saturday, 4 June 2016

NYUMBA 4 KUJENGWA NA WABUNGE WA TANGA KUWANUSURU NDUGU WA MAUAJI YA WATU 8

Wabunge wa majimbo ya Tanga wameamua kuwajengea ndugu wa watu 8 waliouliwa kwa kuchinjwa wiki hii mkoani tanga Nyumba 4. Wabunge hao akiwemo balizi Adadi Rajabu Wa Muheza, Juma Asweso na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wameamua kuwajengea nyumba hizo ndugu hao baada ya kuwakuta hawana pa kuishi. Ndugu hao wamehamia ktk mtaa Zedi Kibatini Jijini humo. Kwa upande wake Balozi Adadi Rajab Ameitaka serikali kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao nchini. Wakizungumza jana kwa Uchungu, wananchi hao wameitaka pia Serikali kuimarisha ulinzi ktk Eneo hilo. Wakaazi ktk mtaa huo wamebomoa makaazi yao ili kunusuru maisha yao baada ya mauaji hayo ya watu 8 yaliohusisha pia kuchinjwa kwa mwenyekititi wamtaa huo.

No comments:

Post a Comment