Tuesday, 14 June 2016

ASKARI ASIYEMPIGIA MBUNGE SALUTI KUKATWA MSHAHARA

Serikali imesema kuwa askari yeyote ambaye hatampigia saluti mbunge atakatwa mshahara wake na adhabu nyingine. Hayo yameelezwa na naibu waziri wa kilimo,mifugo na Uvuvi Wiliam Ole nasha wakati akijibu swali la mmoja wa wavunge wa viti maalum aliyetaka kujua adhabu wapewazo askari kwa kushindwa kuwapigia wabunge saluti, ambapo Naibu waziri Nasha alijibu swali hilo kwa Niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri nasha ameeleza kuwa Askari polisi wote wanapaswa kuwapigia saluti wabunge na viongozi wote kwani saluti ni salam ya kawaida kwa mujibu wa taratibu za jeshi hivyo askari akishindwa kufanya hivyo anatakiwa kuripotiwa kwa mkuu wake wa kazi ili apewe adhabu ikiwemo kufanya usafi katika maeneo yao, paredi na ikiwezekana kukatwa mshahara. Naibu huyo amewataja wengine wanaopaswa kupigiwa Saluti na askari kuwa ni pamoja na Raisi wa Muungano na Zanzibar, Majaji wa Muungano na Zanzibar, Mawaziri na Manaibu wazzi ri wa Muungano na Zanzibar, Spika, Makatibu wa Bunge, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya Zote nchini bara na Visiwani.

No comments:

Post a Comment