Tuesday, 21 June 2016

ICC YAMHUKUMU KIONGOZI WA WAASI NA MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA CONGO( D.R.C) MIAKA 18 JELA

Aliyewahi kuwa kiongozi Wa Waasi na Makamu wa Raisi wa Zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), bwana Jean Pier Bemba amehukumiwa kifungo cha miaka 18 na Mahakama ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita ya Nchini Uholanze (ICC). Taarifa kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa Kiongozi huyo wa Zamani wa DRC, ametiwa hatiani kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo mauaji na Ubakaji. Vitendo hivyo vinadaiwa kufanywa na Jeshi lake katika nchi ya Afrika ya kati, kati ya mwaka 2002 hadi 2003 hulu akishimdwa kulizuia jeshi lake dhidi ya vitendo hivyo vilivyo hatari dhidi ya haki za binadamu. Katika mapigano hayo, jeshi lake lilidaiwa kutekeleza vitendio hivyo kwa raia wa nchi hiyo, hivyo Mahaka ya makisa ya kivita imesema kuwa inamtia hatiani kwa kushindwa kuzuia vitendo hivyo vya kinyama dhidi ya raia. Mahakama hiyo imekuwa ikilaumiwa na viongozi wa Mataifa ya Afrika kwa kile kilichoelezwa kuwaandama sana viongozi wa kiafrika tofauti na mataifa mengine ambapo, wengine waliokwishawahi kushtakiwa kati ka mahakama hiyo ni viongozi wa juu nchini k enya pamoja na Baadhi ya viongozi ktk nchi Ya Sudani. Mawakili wa kiongozi huyo wa zamani wa Congo, wameeleza nia yao ya kukata rufaa dhidi ya hukunu ya mteja wao huyo.

No comments:

Post a Comment