Tuesday, 21 June 2016

CAMEROON AWAONYA RAIA WA NCHI YAKE

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon amewataka raia wa nchi hiyo kufikiria mara mbili kuhusu uwamuzi wao katika kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU). Waziri mkuu Camerooni ameeleza kuwa, raia wa nchi hiyo wanapaswa kufikiria kuhusu hatima ya familia zao na vizazi vijavyo iwapo wataamua kupiga kura ya kujiondoa katika umoja huo kwani wakishaamua hakutakuwa na uwezekano wa kubadili suala hilo. Uingereza inatarajia kupiga kura ya aidha kuamua kubaki au kuondoka katika Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi Wiki hii.

No comments:

Post a Comment