Tuesday, 21 June 2016
UKAWA WATUMIA NJIA NYINGINE KUSUSA KIKAO LEO BUNGENI
Wabunge wa UKAWA wameendelea kususia vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz vinavyoongozwa na Naibu Spika wa Bunge hilo Mh. Dk. Tulia Acksoni.
Leo wabunge hao walitoka bungeni kwa namna ya kimya kimya tofauti na jana walipojiziba midomo kwa karatasi na Plasta. Jana wabunge hao walishindwa kupigia kura bajeti ya serikali kwa kuamua wenyewe kutoka nje ya Bunge.
Leo wametoka kimyakimya huku mwenyekiti mwenza na Mbunge wa Vunjo Jamesi Mbatia akisema Kamati ya uongozi ya wabunge hao watafanya kikao kujua mustakabali wao na watatoa taarifa baadae.
Pamoja na kususa kikao cha kupigia kura ya Bajeti ya Serikali lakini bajeti hiyo ilipita kwa 100% baada ya kupigiwa kura na wabunge 254 kwa wabunge 255 waliokuwepo katika kikao hicho cha bunge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment