Monday, 13 June 2016

HATMA YA PROF. LIPUMBA CUF KUJULIKANA LEO

Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari leo. Katika Mkutano wake huo,Prof. Lipumba anatarajiwa kueleza hatma yake ndani ya chama hicho. Imedaiwa kuwa mazungumzo yake hayo yanatokana na kutokeakwa wimbi kubwa la wanachama ndani ya chama hicho wanaotaka arudi. Vyanzo vya ndani vinaarifu kuwa Mwisho wa wiki Lipumba aliondoa barua yake ya kujiuzulu, hata hivyo haijajulikana kama chama hicho kitamkubakia arudi. Prof. Lipumba aliondoka ktk chama hicho mwishoni mwa mwaka 2015 kwa kile alichodai ni kusutwa na dhamira yakebaada ya UKAWA kumpokeaMh. Lowasa, Wengine waliokasirishwa na uamuzi wa ukawa kumpokea Lowasa ni Dk. Slaa aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema ambaye aliachia madaraka katika chama hicho na hakujiunga na chama kingine cha Siasa.

No comments:

Post a Comment