Monday, 13 June 2016

CHAMA CHA CCK CHAILIPUA CHADEMA..!

Chama cha Kijamii(CCK),kimepinga vikali hatua ya kambi ya upinzani bungeni kutakakumng'oanaibu spika. Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wao wa Taifa bwana akitanda imeeleza kuwa kambi hiyo siku zote umekuwa haitaki kufuata kanuni na hivyo kukorofishana na kiti cha Spika, amesema kuwa Si mara yakwanza kwa wabunge hao kutoka kwabi hata katika bunge la kumi wamekuwa wakitoka, na baadala yake chama hicho kimeitaka kambi hiyo kukaa bungeni na kujadili hoja. Amesema kuwa Naibu Spika ni mbobezi wa kanuni na kwamba kinachofanywa na kambi hiyo ni udhalilishaji wa kijinsia kwa kutakakupiga kura ya kutokuwa na imaninaye, kwani amekuwa akisimamiakanuni kitu ambacho wao hawapendi. Aidha katika taarifa yake hapo jana, ameeleza kuwa kinachotokea kwa wabunge wa upinzani ni kudhani kuwa wanaburuzwa kutokana na uchache wao dhidi ya wale wa CCM. Upinzani umesusia vikao vyote vinavyoongozwa na naibu spika wakidai kupendelea upande mmoja na kuwaminya wao.

No comments:

Post a Comment