Friday, 3 June 2016

HAKI ZA BINDAM WAINGILIA SUALA LA WANAFUNZI UDOM NA WABUNGE WALIOFUKUZWA

Kituo cha haki za Binadam Tz, kimeitaka Serikali kuwarudisha mara moja wanafunzi na Wabunge waliofukuzwa Bungeni. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi Kijobi Simba Imeeleza kuwa Serikali iwarudishe wanafunzi hao na kumaliza suala hilo kwa majadiiano ya amani. Kwa Upande wa Wabunge Mkurugenzi huyo amesema kuwa wanalitaka bunge kuwarudisha wabunge hao mara moja kwani walitenda makosa hayo wakiwa wanawatetea wananchi na kwamba kitendo cha kuwafukuza ni kuwakosesha wananchi haki yao. Aidha ameitaka serikali kuwaadhibu wale wote waliosababisha kuwepo wanafunzi hao baadala ya kuwafukuza wanafunzi.

No comments:

Post a Comment