Friday, 3 June 2016
ACT WAZALENDO WALIKOMALIA BUNGE
Chama cha ACT-wazalendo kimesema kuwa kitafanya maandamano nchi nzima kupinga kufukuzwa kwa Wabunge saba wa upinzani bungeni akiwemo kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe. Taarifa iliyotolewa kwa Waandishi wa habari leo kupitia Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho imeeleza kuwa kwanza watafanya mkutano Tar 5 ktk jiji la Dar kama mapokezi ya kiongozi wao kisha watafanya mikutano mingine Mbeya na Kigoma. Chama hicho kimesema kuwa kitendo cha kufukuzwa wabunge wao Sio kizuri kwani kinaminya Demokrasia na kwamba ktk mikutano hiyo kiongozi wao Zitto anatarajia kueleza mustakabali wa Siasa ya TZ. Aidha ACT kimesema kuwa tayari wameshawaandikia Chadema, CUF na NCCR kuona kama wataungana ila hawajapokea majibu Bado. Wiki hii Wabunge saba waupinzani walipewa adhabu ya kutohudhuria vikao mbalimbali bungeni mjini Dodoma baada yakupatikana na hatia ya kufanya vurugu bungeni Mwezi Januari wakati wa Mjadala wa kutorushwa mojakwa moja matangazo ya Bunge. Waliokumbwa na dhahama hiyo mi Zitto, Lisu, Bulaya, Mdee, Lema Paulina Gekul na John Heche.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment