Thursday, 30 June 2016
WAUAJI WA TANGA WAUAWA NA POLISI
Polisi mkoani Tanga imesema kuwa imewaua watu 3 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya watu nane kwa kuwachinja katika mtaa wa Kibatini Kata ya Mzizima Jijini Tanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Kamishina Msaidizi wa Polisi Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa Majambazi hayo yaliuawa kwa kushirikiana na vikosi vya majeshi ya ulinzi na yale ya usalama,(vikosi vya polisi na JWTz).Kamanda Paul ameeleza kuwa majambazi hayo yaliuawa katika maeneo ya mapango katika msitu ulioko katika Maeneo ya Mapango ya Amboni jirani na eneo la Mauaji hayo baada ya majambazi kuwafyatulia Risasi Askari baada yakuona yanazidiwa nguvu. Hata Hivyo vikosi vya ulinzi vilifanikiwa kuyakabili majambazi hayo na kuyapiga risasi ktk majibizano na hatimaye kufariki yakiwa yanakimbizwa hospitalini. Wiki hii jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar ,liliripoti kumuua kiongozi wa mauaji hayo.
Katika msako huo, Vikosi vya ulinzi na usalama vilifanikiwa kukamata bunduki 2 aina ya SMG, bastola 1 , risasi 30 pamoja na visu na Majambia yaliotumika kuwachinja watu nane mwezi uliopita katika Mtaa huo.
Jeshi la polisi limewahakikishia wakaazi wa eneo hilo kuwa hali iko salama baada ya kuhakikisha maficho ya majambazi hayo yamedhibitiwa ipasavyo katika msako unaoendelea katika kuwasaka majambazi hayo na kukomesha kabisa uhalifu katika jiji la Tanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment