Thursday, 16 June 2016

CCM YAMJIBU GWAJIMA

Chama cha mapinduzi kimesema kuwa kimesikitishwa sana na kitendo cha Mchungaji wa Kanisa la Ufuofuo na uzima Josephat Gwajima kwa kukizushia uongo chama hicho kuwa kinampango wa kutompa raisi Magufuli uwenyekiti. Taarifa iliotolewa na msemaji wa Chama hicho Bw, Ole Sendeka imeeleza kuwa maneno ya mchungaji huyo ni ya uongo na kwa wanachamba na wapenzi wanapaswa kuyapuuzia kwani Gwajima hajawahi kuitakia mema ccm na uongozi wake na baadala yake amekuwa akipigia kampeni chama chake cha upinzani ili kishinde na kwamba Msemaji huyo ameeleza kuwa hizo ni mbinu za Gwajima kuidhoofisha ccm ili chama chake kishinde kitu ambacho hakitawezekana ksmwe. Ole Sendeka amemtaka mchungaji huyo kama anaushahidi awataje watu hao na sio kueneza fitina na uchochezi kwq rais na Chama chake. Ole Sendeka ameeleza kuwa Kitendo cha Gwajima kumuambia Rais ahame ni kutoitakia ccm mema na Rais Pia kwani kwa mujibu wa katiba raisi lazima awe na chama hivyo rais akihama makamu wa rais anashika nafasi na kazi inaendelea. Olesendeka amesema kuwa Rais Magufuli yuko imara hata danganyika na mbinu chafu za Gwajima kama alivyo mdanganya bwana mmoja ahame ccm akimnadi kuwa atakuwa raisi na bwana huyo kushindwa na kwa sasa wameanza kumkimbia. Juzi Gwajima ktk mahubiri yake alisema kuna watu wanazunguuka nchi nzima kuwashawishi wanaccm kutenganisha kati ya urais na uwenyekiti wa chama ili Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.

No comments:

Post a Comment