Monday, 20 June 2016
GAZETI LA DIRA LATAKIWA KUOMBA RADHI MARA MOJA NA JWTZ.
Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tz (JWTZ),limelitaka gazeti la Dira la leo kuomba radhi mara moja kwa sababu za kuandika habari ya uongo kuwa kifaru cha jeshi hilo kikosi cha 83 KJ kimeibiwa katika mkoa wa Pwani. Taarifa iliotolewa na msemaji wa Jeshi hilo leo Kanali Ngemela Lubenga imeeleza kuwa, taarifa hizo ni za uongo na kwamba usalama katika maeneo ya makambi ya Jeshi unaimarishwa sana kiasi kwamba ni vigumu kutokea kwa tukio hilo. Kanali Ngemela ameeleza kuwa Jeshi limesikitishwa sana na taarifa hiyo kwani inaharibu taswira ya Jeshi hilo hapa Tz na Duniani kwa Ujumla. Msemaji huyo wa Jeshi ameongeza kuwa jeshi la Ulinzi la Tz, limekuwa likiheshimika duniani na Afrika kutokana na kushiriki katika shughuli mbalimbali za ukombozi wa nchi za Afrika hivyo habari hiyo imelichafulia taswira jeshi hilo. Aidha kanali huyo amewaasa waandishi wa habari kuwa makini na habari zisizo naukweli juu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tz, na kwamba gazeti hilo limetakiwa kuomba radhi la sivyo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment