Tuesday, 14 June 2016
LIPUMBA APIGWA STOP KURUDI CUF.
Wakati Prof. Ibrahim Lipumba aliyekuwa mwenyekiti wa CUF akitangaza kuwa amemuandikia katibu mkuu wa chama hicho barua ya kutengua uamuzi wake wa kung'oka kwenye uwenyekiti wa chama hicho, viongozi wa juu wamekataa kwa kusema katiba yao hairuhusu na kwamba huo ni mpango wa kutaka kurudi kuiua CUF kabisa ulioandaliwa na kiongozi huyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao ambao ni makam mwenyekiti Twaha Taslima na Kaimu katibu mkuu Zanzibar Nasoro Mazrui wamesema kuwa hawatamkubalia arudi kwa kuwa matatizo aliyokimbia hakuna lililoondoka bado yapo palepale. Viongozi hao wameenda mbali na kudai kuwa huo ni mpango wa CCM kumtumia ili akimalize chama chao kabisa. Kwa upande wake Taslima ameeleza kuwa toka Lipumba aondoke wamepambana na changamoto nyingi sana hadi chama kimetengemaa sasa hawana haja na Lipumba tena.
Lipumba alijiondoa kwenye chama hicho mwezi August 2015 kwa kile alichoeleza kusutwa na nafsi yake baada ya ukawa kumpokea Lowasa. Jana Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kudai kuwa ameiandikia CUF barua kupitia kwa katibu mkuu kuomba kurudi kwenye wadhifa wake akidai kuwa hapendezewi na hali ya kidemokrasia nchini ikiwemo suala la uchaguzi wa Zanzibar, hivyo anataka kurudi kuendeleza mapambano kitu kilichopingwa vikali na viongozi wa juu wa CUF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment