Monday, 13 June 2016

ZITTO KABWE APATIKANA.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto kabwe aliyeripotiwa na chama chake kupotea tangu juzi amepatikana leo. Zitto alijitokeza leo na kusema kwamba polisi walikuwa wanamsaka ila hawajafanikiwa kumkamata. Zitto amesema kuwa watu wa usalama wa chama chake walihakikisha hakamatwi kwa kanuni zao bali kwa utaratibu wa nchi. Zitto hajaeleza alikokuwa tokakutoweka kwake juzi jioni ambapo jana alitarajiwa kuwa msemaji mkuu katika kongamano la chama chake la kuchambua bajeti ya serikali 2016/17 kabla ya kongamano hilo kupigwa marufuku kwa kukosa kibali.

No comments:

Post a Comment